Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la wizi wa mabati Uganda lahusisha mawaziri 22

Sakata La Wizi Wa Mabati Uganda Lahusisha Mawaziri 22 Sakata la wizi wa mabati Uganda lahusisha mawaziri 22

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Kashfa ya mawaziri 22 kuhusishwa na kile kinachoelezea kuwa wizi wa mabati ya jamii ya watu masikini wa Karamoja ni mojawapo ya vitendawili kwa rais Yoweri Museveni katika vita vyake dhidi ya ufisadi miongoni mwa baraza lake la mawaziri.

Watu mbalimbali wanaelezea kashfa hii kuwa kielelezo cha uozo wa maadili kuanzia ngazi za juu serikalini na kupelekea jambo la ufisadi na ulaji rushwa kwa jumla kuwa la kawaida Uganda.

Kulingana na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa, hatua za kuanza kuwakamata baadhi ya mawaziri si suala litakalokubalika kuwa sasa Museveni amedhihirisha kwamba anapigana dhidi ya ufisadi.

Hadi pale mawaziri na vigogo kama vile spika watakapokamatwa na kufunguliwa mashtaka hapo ndipo taifa litakubali kuwa kweli makali ya Museveni kupambana na ufisadi ni ya uhakika.Lakini kukamatwa kwa wale ‘samaki wadogo na kuwaacha papa’ itakuwa mzaha tu.... hiyo ni kauli ya mwanaharakati mmoja.

Lakini Museveni amejikuta kwenye njia panda kwani mawaziri nyeti katika serikali yake wamekiri waziwazi kupokea shehena za mabati hayo yaliyokusudiwa wafugaji wa kuhamahama ili wabadili maisha yao.

Miongoni mwao ni waziri mkuu, waziri wa fedha, spika wa bunge, naibu wa kwanza wa waziri mkuu na wengineo. Akigusia suala hilo alipohutubia wananchi kaskazini magharibi mwa nchi, Museveni alitaja kashfa hiyo kuwa ufisadi wa kisiasa na unastahili adhabu za kisiasa vilevile. Adhabu za kisiasa kwa kawaida ni kumfuta waziri.

Lakini je Museveni atamfuta nani amwache nani miongoni mwa mawaziri wake hao 22.

Tayati mawaziri 3 wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka na kisha kusukumwa rumande gerezani.

Kulingnana na taarifa za ofisi ya kiongozi wa mashtaka wameandaa kesi 8 dhidi ya washukiwa ila haijabainika ni akina nani hasa watawafuata wale mawaziri watatu.

Wawili kati ya waliofikishwa ni mawaziri wa Karamoja wenyewe na mwingine ndiye alitumia mabati hayo kuezeka mabanda ya mbuzi na kuku wake.

Matumizi hayo yameshangaza wananchi wakielezea kuwa huo ni wizi wenye dharau kubwa kwa maslahi ya umma.

Waziri wa fedha aliibua vioja aliposema kuwa aliyakuta mabati nyumbani kwake bila kuyaomba akadhani ni zawadi kwa watu anaowakilisha bungeni.

Baadhi ya mawaziri wameamua kurudisha mabati hayo au kufidia kwa kununua mengine na kuyarudisha.

Lakini mwa mtazamo wa wananchi, kurudisha mabati si kwamba huna hatia. Spika wa bunge na mawaziri wengine wanne wamefanya hivyo.

Chanzo: Bbc