Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la waomba hifadhi Rwanda lapunguza kasi ya wahamiaji Uingereza

Rwanda Wakimbizi Ndege Sakata la waomba hifadhi Rwanda lapunguza kasi ya wahamiaji Uingereza

Wed, 22 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa mkuu katika Ofisi ya Mambo ya Ndani ya Uingereza anasema sera ya kuwapeleka wahamiaji Rwanda inaweza kuwa ilipunguza mtiririko wa wahamiaji kuelekea Uingereza.

Matthew Rycroft aliwaambia wabunge kuwa idadi ya wanaovuka ni ya juu ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu - lakini chini ya makadirio ya idara hiyo.

“Tayari kuna uwezekano kuwa matokeo yake yameanza kujitokeza,” Bw Rycroft aliiambia kamati teule ya mambo ya ndani.

Pia alifichua kuwa watu 47 walikuwa wameambiwa wangeondoka kwa ndege ambayo ilipangwa wiki iliyopita - na kisha ikafutwa, wakati changamoto za kisheria zilizuia waomba hifadhi kuondolewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live