Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saini ya Buhari ilighushiwa ili kutoa $6m, mahakama yaambiwa

Saini Ya Buhari Ilighushiwa Ili Kutoa $6m, Mahakama Yaambiwa Saini ya Buhari ilighushiwa ili kutoa $6m, mahakama yaambiwa

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Nigeria inatafuta usaidizi wa Interpol ili kuwakamata washukiwa watatu wanaodaiwa kuiba $6.2m (£4.9m) kutoka kwa benki kuu, kwa kutumia sahihi iliyoghushiwa ya Rais wa wakati huo Muhammadu Buhari.

Mamlaka zinaamini kuwa washukiwa hao walikula njama na aliyekuwa mkuu wa benki kuu ya Nigeria Godwin Emefiele.

Tayari anakabiliwa na mashtaka 20, ikiwa ni pamoja na kupokea $6.2m kinyume cha sheria.

Bw Emefiele amekana mashtaka yote, na kwa sasa yuko nje kwa dhamana.

Yeye ndiye afisa wa zamani mwenye hadhi ya juu zaidi kushtakiwa kwa ufisadi tangu Rais Bola Tinubu aingie madarakani Mei mwaka jana.

Waendesha mashtaka pia wanadai kuwa Bw Emefiele aliidhinisha kinyume cha sheria kutolewa kwa pesa hizo kutoka kwa hazina ya benki kuu.

Katika taarifa yake Desemba mwaka jana, alitaja madai hayo kuwa "uongo mtupu uliosemwa na mpelelezi ili kufanikisha ajenda yake ya kishetani".Alitoa wito wa "uchunguzi wa kina na wa uwazi".

Watu wanaodaiwa kuwa washirika wa Bw Emefiele wametajwa kuwa ni Adamu Abubakar, Imam Abubakar na Odoh Ocheme, mfanyakazi wa zamani wa benki kuu, Shirika la Habari linalomilikiwa na serikali la Nigeria liliripoti.

Washukiwa hao wanaaminika kuondoka Nigeria, jambo lililosababisha mamlaka kutafuta usaidizi wa Interpol kuwakamata na kuwarejesha makwao, shirika hilo liliongeza.

Chanzo: Bbc