Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari za ndege zatatizika baada ya ndege kutua kwa ghafla Nigeria

Safari Za Ndege Zatatizika Baada Ya Ndege Kutua Kwa Ghafla Nigeria Safari za ndege zatatizika baada ya ndege kutua kwa ghafla Nigeria

Mon, 8 May 2023 Chanzo: Bbc

Safari kadhaa za ndege zimesitishwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe katika mji mkuu wa Nigeria Abuja baada ya ndege kutua kwa dharura na kuziba njia ya ndege kurukia.

Ndege ya Max Air 737-400 ilipasuka tairi siku ya Jumapili ilipotua Abuja, kutoka Yola, kaskazini-mashariki mwa jimbo la Adamawa.

Uongozi wa Max Air ulisema kuwa abiria wote 143, mtoto mchanga na wafanyakazi sita waliokuwemo ndani ya ndege hiyo waliondolewa salama bila majeruhi.

Tukio hilo limesababisha kuahirishwa kwa safari nyingi na ucheleweshaji kote nchini, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Mamlaka ilisema ndege hiyo iliondolewa Jumapili jioni na njia ya kurukia ndege ilikuwa ikikaguliwa na kufagiliwa ili kufunguliwa tena.

Abiria wengi wameripotiwa kukwama katika uwanja huo wa ndege.

Chanzo: Bbc