Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari ya Ikulu: Bwenyenye Jimmy Wanjigi atangaza kuwania urais 2022

19cdb4d3771d1f6e Safari ya Ikulu: Bwenyenye Jimmy Wanjigi atangaza kuwania urais 2022

Wed, 16 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wanjigi ana mifuko mizito na sasa amesema 2022 kila mtu ajifadhili kwani hata yeye anataka kuonja vya IkuluAmekuwa akiwafadhili wanasiasa kama vile Uhuruto 2013 na NASA 2017 na kisha kupata usemi serikaliKivumbi cha 2022 kinaendelea kuwavutia wengi huku Rais Uhuru Kenyatta naye akiwasha moto kwa kusema ataunga mkono NASABwenyenye Jimmy Wanjigi ametanagaza kuwa anamezea mate kiti cha urais na anajiandaa kuingia Ikulu 2022.

Wanjigi amekuwa akiwafadhili wanasiasa wakuu humu nchini lakini sasa amesema ni wakati wake kufurahia minofu ya Ikulu pia.

Wanjigi anajulikana kwa kuwa na mifuko mizito na kila kigogo anayetafuta mapeni ya kuendesha kampeni za kuingia Ikulu hubisha kwake.

Akiongea na gazeti la Standard, alsiema yeye ni mjuaji wa siasa za Kenya na amekuwa akisoma karata ambayo huchezwa hadi mtu kuingia ikulu.

"Wakati huu sitakuwa nikimfadhili yeyote. Na maswali yenu nitayajibu wakati mwafaka ukifika," alisema kigogo huyo.

Baadaye aliiambia runinga ya NTV kuwa tayari amevua nguo kuyaoga maji ya Ikulu kwenye kinyang'anyiro hicho ambapo ni wazi mambo yatakuwa kivumbi.

"Wacha nidhibitishe kuwa nitakuwa kwenye siasa zijazo na wala si kama awali ambapo nimekuwa nikiwasaidia wengine," alisema tajiri huyo kutoka Murang'a.



Amekuwa kwenye siasa kwa muda ambapo 2013 alifadhili muungano wa William Ruto na Uhuru Kenyatta kuingia serikalini.

Kulingana na duru zinazomjua Wanjigi, yeye ni sungura wa siasa za Kenya na hufungua mikoba yake kwa walio na nafasi ya kuingia Ikulu.

Wakipata ushindi, huwa ana usemi mkubwa ambapo hufaidika na tenda za mabilioni ya fedha na hivyo kujijenga kama mfanyibiashara.

Marafiki wake huwa ni wafanyibishara wengine wazito kama vile mwendazake Jacob Juma ambaye waliingia naye NASA kwenye kinyang'anyiro cha 2017.

Waliwekeza kwenye muungano huo na Wanjigi amekuwa ni rafiki wa karibu wa kinara wa ODM Raila Odinga.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke