Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za kukamatwa Msaidizi wa Rais Mstaafu wa Zambia

Amoszambia.png Sababu za kukamatwa Msaidizi wa Rais Mstaafu wa Zambia

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msaidizi wa Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu amekamatwa na kushtakiwa kwa kuwatusi na kuwazuia maafisa waliokuwa wakipekua nyumba yake.

Msemaji wa Rais huyo wa zamani, Amos Chanda alikamatwa na kushtakiwa pamoja na mkewe na shemeji yake waliokuwepo wakati wa tukio hilo.

Bwana Chanda alihojiwa kwa saa nane kabla ya kufunguliwa mashtaka na kuachiliwa kwa bondi.

Watatu hao wanadaiwa kuwatusi na kuwazuia maafisa wa kukabiliana na ufisadi waliokuwa wakiendesha msako nyumbani kwao.

Mpaka sasa Chanda hajazungumza lolote kuhusu mashtaka hayo lakini wakati wa msako huo, aliwashutumu maafisa hao kwa uwindaji wa wachawi akisema hakufanya kosa lolote.

Kumekuwa na tuhuma za ufisadi zinazotolewa dhidi ya viongozi katika utawala wa Rais wa zamani Lungu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live