Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za Diane kung'olewa uchaguzi Rwanda

Diane Shima Rwigara Kagame.jpeg Diane Rwigara na Kagame

Sat, 8 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Rwanda, Oda Gasinzigwa amesema jina la Diane Rwigara (42) ambaye ni kiongozi wa vuguvugu la People Salvation halijapitishwa katika kinyang’anyiro cha wagombea urais nchini humo kwa sababu ameshindwa kutoa hati inayothibitisha kuwa ana asili ya Rwanda. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).

Pia amesema mwanamama huyo ambaye katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 pia alikataliwa kugombea urais, ameshindwa kuwasilisha taarifa ya rekodi ya uhalifu kama inavyoagizwa na tume ya uchaguzi na badala yake akatoa nakala ya hukumu ya mahakama.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mkuu huyo wa tume pia ameongeza kuwa; “Kuhusu sharti la kupata uidhinishaji wa saini za watu 600, hakutoa angalau saini 12 kutoka wilaya nane.”

Rwigara alikataliwa kugombea mwaka 2017 kwa tuhuma za kughushi saini za wafuasi wake kwa ajili ya fomu yake.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 42 alikamatwa, na kushtakiwa kwa kughushi na kuchochea uasi na kufungwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kuachiliwa huru mwaka 2018.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame atakabiliana na wapinzani wawili katika uchaguzi wa mwezi ujao, kulingana na orodha ya muda ya wagombea urais iliyochapishwa jana Alhamisi.

Gasinzigwa amewataja Kagame, Frank Habineza wa chama cha Democratic Green Party na mgombea huru Philippe Mpayimana kama wagombea katika uchaguzi wa tarehe 15 Julai mwaka huu.

Wote Habineza na Mpayimana walikuwa pia wagombea pekee walioruhusiwa kushindana na Kagame katika uchaguzi wa mwaka 2017.

Gasinzigwa alisema katika tangazo kwenye televisheni ya serikali kwamba jumla ya fomu tisa za wagombea watarajiwa zilipokelewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live