Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za Afrika Kusini kumpeleka Marekani Waziri wa Fedha wa Msumbiji

Manuel Chang Will Face Corruption Charges In U S Sababu za Afrika Kusini kumpeleka Marekani Waziri wa Fedha wa Msumbiji

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: New York Times

Mahakama ya Afrika Kusini imeamuru kwamba aliyekuwa waziri wa fedha Manuel Chang anapaswa kupelekwa nchini Marekani ambapo anasakwa kwa makosa ya uhalifu kuhusiana na kashfa kubwa ya ufisadi.

Uamuzi wa mahakama hiyo unafutilia mbali uamuzi wa waziri wa haki nchini Afrika Kusini Ronald Lamola mwezi Agosti kumhamisha Chang katika nchi yake.

Jaji wa mahakama kuu Margaret Victor alisema mahakama haikupata uamuzi huo kuwa unaokubalika.

Makundi ya wanaharakati yalipinga kumhamisha Chang kuelekea Msumbiji akihofia kwamba asingekabiliwa na mashtaka.

Waziri huyo wa zamani amekuwa kizuizini nchini Afrika kusini tangu 2018kutokana na agizo la kumkamata kwa madai ya kutaka kufanya ulaghai na utakatishaji wa fedha.

Kashfa hiyo inahusisha zaidi $2.7bn (£2bn) za deni la serikali lisilojulikana ambalo serikali iliomba ili kujenga kiwanda cha samaki , kununua wavu wa kuvulia samaki na mabotoiya kijeshi ili kuweka usalama , lakini kiwango kikubwa cha fedha hizo zilidaiwa kugawanyiwa maafisa wafisadi.

Chang, 66alikana kukubali $7m kama hongo. Alikamatwa kufuatia ombi la Marekaniambapo wawekezaji waliathiriwa na kashfa hiyo.

Chanzo: New York Times