Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya mafuriko makubwa Nigeria na Niger

Mafuriko Nigeria Sababu ya mafuriko makubwa Nigeria na Niger

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Utafiti mpya umebaini kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yalizidisha mvua kubwa zilizosababisha mafuriko makubwa katika maeneo ya Nigeria na Niger mwaka huu na kuua mamia ya watu.

Mafuriko hayo yalirekodiwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika nchi hizo mbili.

Ripoti ya shirika la World Weather Attribution inasema mvua kubwa za msimu na kutolewa kwa maji kutoka kwenye mabwawa kulisababisha mafuriko kuanzia Juni hadi Oktoba.

Walihitimisha kuwa tukio hilo lilifanywa mara 80 zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Takriban watu milioni 1.5 waliachwa bila makao, mamia kwa maelfu ya nyumba zilisombwa na maji na zaidi ya hekta nusu milioni za mashamba ziliharibiwa na mafuriko hayo.

Utafiti mpya umebaini kuwa mabadiliko ya tabia nchi yalizidisha mvua kubwa zilizosababisha mafuriko makubwa katika maeneo ya Nigeria na Niger mwaka huu na kuua mamia ya watu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live