Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya Uganda kupiga marufuku usafirishaji mali ghafi nje ya nchi

Uganda Fortification Photo01 Sababu ya Uganda kupiga marufuku usafirishaji mali ghafi nje ya nchi

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wiki iliyopita Wizara ya Baishara, Viwanda na Ushirikiano ilipiga marufuku usafirishaji wa malighafi zote kutoka ndani ya nchi hiyo kwenda nchi za nje kuanzia mwaka mpya wa fedha.

Kwa mujibu wa wizara hiyo ni kwamba maamuzi hayo yamechukuliwa ili kupunguza hasara inayotokana na usafirishaji wa bidhaa ghafi kabla hazijaongezwa thamani.

Waziri wa Baishara Bi. Harriet Ntabazi, amesema takribani asilimia 69, ya mali ghafi kutoka Uganda husafirishwa kwenda nje ya nchi kila mwaka na kupelekea nchi kupoteza mapato, hivyo uamuzi huo utaongeza kasi ya uzalishaji bidhaa za ndani.

Wizara hiyo pia imefanikiwa kupata mkopo wa dola za Marekani Milioni 29 kutoka wadau wa maendeleo na pia imetoa dola za Marekani milioni 29 kwenda Bank ya Maendeleo ya Uganda kwaajili ya kusaidia wafanyabiashara.

Waziri Harriet amesema ongezeko la kodi limeathiri wafanyabiashara pia athari za ugonjwa wa Corona pamoja na kufungwa nchi kutokana na janga hilo kumepelekea kuyumba kwa sekta ya biashara.

Waziri huyo pia amelaumu ongezeko la kodi ya mavazi kutoka 25% hadi 33% kulikofanywa na wizara ya fedha, na kudai kwamba ongezeko hilo litaathiri pande zote ndani na nje.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live