Rais William Ruto bado hajahamia katika Ikulu licha ya mtangulizw wake, Uhuru Kenyatta kuondoka kwenye makao hayo rasmi ya kiongozi wa taifa.
Inadaiwa kwamba Ruto alikuwa akitumia Ikulu kufanyia mikutano yake akiwa Rais, ila kuamua kurejea kwenye makao yake ya Karen kulala.
Duru za kuaminika zinaarifu kuwa Ruto aliamua kusalia Karen katika makao rasmi ya Naibu Rais, kwa sababu Ikulu kwa sasa inafanyiwa ukarabati kwa jinsi itakavyomfurahisha.
Rais William Ruto bado hajahamia katika Ikulu ya Nairobi, licha ya mtangulizi wake Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuondoka kwenye makao hayo rasmi ya kiongozi wa taifa.
Mabadiliko Aliyofanya Rais William Ruto Alipochukua Usukani Katika Ikulu Ukarabati huo unatarajiwa kuchukua kipindi cha miezi mitatu hivi, ila hautaathiri kivyovyote utendakazi wake akiwa kiongozi wa nchi.
"Ukarabati wa Ikulu umeanza na huenda ukachukua miezi mitatu kabla ya Rais kuhamia pale, haswa upande wa kuishi. Kwa sasa, ataendelea kutumia ofisi za Ikulu huku akiishi Karen," mwandani wa karibu wa Ruto aliiambia jarida la the Standard.
Ruto alibadilisha samani za Ikulu, zikiwemo viti ambavyo vilivyokuwa vikitumika awali na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.
Vile vile alibadilisha akaunti za mitandao ya kijamii za Ikulu na kmuweka picha zinazohusishwa na uongozi wake mpya.