Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya Niger kuvunja uhusiano wa kijeshi na Marekani...

Wanajeshi Wa Ufaransa Wataondoka Niger Ifikapo Disemba 22 Sababu ya Niger kuvunja uhusiano wa kijeshi na Marekani...

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Niger iliamua kusitisha makubaliano ya kijeshi na Marekani baada ya ujumbe wa maafisa wakuu wa kijeshi wa Marekani kuitembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi na "kueleza wasiwasi" kuhusu uhusiano wake na Russia na Iran unaokua

Pentagon ilisema Jumatatu kwamba maafisa hao walisafiri hadi mji mkuu wa Niamey wiki iliyopita ili kujadili suala hilo na uongozi wa kijeshi wa nchi hiyo, wakitaka ufafanuzi kuhusu mipango ya baadaye.

Msemaji wa Pentagon Sabrina Singh alidai kuwa serikali ya Marekani ilikuwa na mazungumzo ya "moja kwa moja na ya wazi" nchini Niger, na inaendelea kuwasiliana na baraza tawala la kijeshi la nchi hiyo - linalojulikana kama Baraza la Kitaifa la Ulinzi wa Nchi (CNSP).

Singh amesema: "Maafisa wa Marekani walionyesha wasiwasi wao juu ya uwezekano wa uhusiano wa Niger na Russia na Iran."

Serikali ya Niger ilitangaza siku ya Jumamosi kwamba imefuta makubaliano ya ushirikiano wa ulinzi wa 2012 na Marekani.

Uamuzi huo umechukuliwa siku chache baada ya ujumbe wa ngazi ya juu wa Marekani, uliojumuisha Mkuu wa Kamandi ya nchi hiyo barani Afrika, Jenerali Michael Langley, kukamilisha ziara yake ya siku tatu katika taifa hilo la Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live