Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya Joho kujindoa kwenye mbio za Urais 2022

4b2c0169c224b4b2 Sababu ya Joho kujindoa kwenye mbio za Urais 2022

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Gavana wa Mombasa Hassan Joho ametangaza kwamba hatawania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022 kama alivyokuwa amesema awali.

Gavana Joho amesema amemuachia kinara wa chama cha ODM Raila Odinga nafasi hiyo akiwa na matumaini kwamba wakati huu ataibuka mshindi.

Joho amesema badala yake amemuachia kinara wa chama cha ODM Raila Odinga nafasi hiyo akiwa na matumaini kwamba wakati huu ataibuka mshindi.

Akizungumza siku ya Jumamosi, Septemba 17 akiwa mjini Mombasa, Joho alisema iwapo Raila atakuwa Rais, basi wakazi wa eneo la Pwani watanufaika sana kutoka na uongozi wake.

" Niko tayari kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais, sio eti kwa sababu naogopa bali naamini kwamba njia ya kipekee sisi kama wakazi wa Pwani kuingia Ikulu ni kupitia kwa kinara wa chama cha ODM Raila Odinga." Joho alisema.

Read also

Magazeti Jumanne, Septemba 21: Raila Aabiri Rasmi Gari la Kuingia Ikulu

Akitoa tangazo hilo, Joho aliwarai viongozi wa chama cha ODM kuwakumbuka viongozi kutoka eneo la Pwani kwa kuwapa nyadhifa za juu katika serikali ijayo.

" Namuomba Raila kuwakumbuka viongozi kutoka eneo la Pwani, hatutakia kuendelea kuwa nje ya serikali, hatuta kikutizama uongozi kwa umbali, tunataka pia kuwa sehemu ya serikali kuanzia sasa hivvi," Joho alisema.

Kwa mujibu wa taarifa za Daily Nation, Joho alijiondoa kinyang'anyironi baada ya kuahidiwa kazi nono na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.

Wakiwa kwenye mkutano wa faragha Raila, Joho na viongozi wengine kutoka Pwani, walijadili jinsi watakavyopata nafasi katika seneti, bunge na katika wizara mbali mbali.

Viongozi kutoka Pwani walighadhabishwa kwamba eneo la Pwani huwa linapewa tu nyadhifa za utalii pekee ambazo huwa nadra kwa wengi wao kuzipata.

Kwa hivyo, wamemtaka Raila kuwakumbuka kwa nafasi nono endapo atachaguliwa kuwa Rais 2022.

" Bado tunafanya mazungumzo lakini mipango imeshika kasi, tunataka Joho apewe nafasi nono nchini," Mbunge wa Ganze Teddy Mwambire alinukuliwa na Daily Nation.

Read also

Jimi Wanjigi Afichua Kile Atakachokifanya Iwapo Raila Atamshinda Katika Uteuzi wa Chama

Kulingana na Mwambire, wakati huu viongozi wa Pwani wanataka nyadhifa kama ya uspika wa bunge, spika wa seneti katika serikali ijayo.

Kwa sasa wanasiasa ambao bado wanakimezea kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha ODM ni gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya na mfanyabiashara Jimi Wanjigi.

Wanjigi ameapa kwamba lazima awe debeni ikizingatiwa kwamba amekuwa akimuunga mkono na kmfadhili Raila kwa miaka kadhaa, kwa hivyo amemtaka arudishe mkono.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke