Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saba wapoteza maisha, Mamia wayahama makazi yao

Sudan Mafuriko Sudan ya Kusini

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: VOA

Mamlaka ya Jimbo Unity Sudan kusini,imesema kuwa takriban watu 7 wamepoteza maisha baada ya mafuriko kusomba nyumba zao kwenye eneo la Mayendit huku familia takriban 400 zikilazimika kuhama makazi yao.

Mkuu wa kaunti ya Mayendit, Gatluak Nyang ameliambia Shirika la Habari la VOA,mvua kubwa zimeendelea kunyesha katika wiki kadhaa zilizopita,na watu 7 wanasemekana kufa maji kutokana na mafuriko.

Amesema takriban asilimia 90 ya ardhi ya Mayendit imefunikwa na maji ambayo pia yameuwa zaidi ya ng'ombe 500 na mbuzi 300. Aidha, Nyang amesema kuwa watu wengi wanateseka kutokana na magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa mazingira safi, pamoja na malaria kutokana na kuwa hawana neti za kujikinga na mbu.

Mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada yameombwa kuingilia kati na kupeleka misaada muhimu ya kibinadamu katika eneo hilo.

Chanzo: VOA