Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SUDAN: Jeshi laahidi kurejesha utawala wa kiraia

Sudan Amani Amani Jeshi laahidi kurejesha utawala wa kiraia

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan ametangaza kuwa atalivunja baraza huru analoliongoza na kukabidhi madaraka kwa serikali mpya ya mpito.

Lakini Jenerali Abdel Fattah Burhan hakutoa ratiba ya kipindi ambapo makabidhiano yatafanyika au jukumu ambalo jeshi litakuwa nalo katika muundo uliopendekezwa.

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni, Jenerali Burhan pia alitangaza kwamba jeshi halitahusika tena katika mazungumzo ya kumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo, huku nafasi yake katika mazungumzo ikichukuliwa na mashirika ya kiraia.

Ni hatua ya kubwa kwa kiongozi huyo kuonekana kulegeza kamba tangumaandamano ya kudai demokrasia kutoka kwa raiawanaotaka jeshi kuachilia madaraka Jeshi lilichukua mamlaka katika mapinduzi ya Oktoba mwaka jana baada ya kupindua serikali ya kiraia ya Waziri Mkuu Abdalla Hamdok.

Tangu wakati huo, muungano wa madaktari unasema zaidi ya watu 110 wameuawa katika maandamano ya kupinga mapinduzi.

Wiki iliyopita, watu 9 waliuawa na vikosi vya usalama wakati wa siku mbili za maandamano ambayo yamekuwa makubwa zaidi tangu jeshi lichukue mamlaka mnamo Oktoba 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live