Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SADC: Uchaguzi Zimbabwe haukufuata misingi ya kidemokrasia

SADC: Uchaguzi Zimbabwe Haukufuata Misingi Ya Kidemokrasia SADC: Uchaguzi Zimbabwe haukufuata misingi ya kidemokrasia

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: Voa

Mkuu wa SADC, Nevers Mumba alisema hata hivyo ujumbe huo umeona kwamba baadhi ya vipengele vya uchaguzi uliowiana kulikuwa na upungufu kulingana na katiba ya Zimbabwe, sheria ya uchaguzi na misingi ya SADC na miongozo inayosimamia uchaguzi wa kidemokrasia

Waangalizi wa uchaguzi kutoka jumuiya ya kikanda ya kusini mwa Afrika (SADC) wamesema uchaguzi wa rais na wabunge nchini Zimbabwe haukufuata misingi ya kidemokrasia.

Ujumbe huo ulibaini kuwa awamu za kabla ya uchaguzi na upigaji kura, kulikuwa na amani na utulivu. Hata hivyo umeona kwamba baadhi ya vipengele vya uchaguzi uliowiana kulikuwa na upungufu kulingana na katiba ya Zimbabwe, sheria ya uchaguzi na misingi ya SADC na miongozo inayosimamia uchaguzi wa kidemokrasia, alisema mkuu wa ujumbe huo Nevers Mumba.

Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SACD) imetaja kufutwa kwa mikutano ya upinzani na shutuma za kunyanyaswa kwa wapiga kura ni miongoni mwa baadhi ya masuala yaliyovuruga uchaguzi.

Uchaguzi huo unaangaliwa kote kusini mwa Afrika kama mtihani wa uungaji mkono kwa chama cha Rais Emmerson Mnangagwa cha ZANU-PF ambacho utawala wake wa miaka 43 umekumbwa na uchumi ulioporomoka na madai ya utawala wa kimabavu.

Chanzo: Voa