Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SADC: Nchi wanachama zatakiwa kushirikiana kupambana na athari za ukame

Ukamee Data SADC: Nchi wanachama zatakiwa kushirikiana kupambana na athari za ukame

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, wiki hii ameyataka mataifa ya kusini mwa Afrika kutumia rasilimali zao kuzisaidia nchi zinazokabiliwa na hali ya ukame kwenye ukanda.

Wito wake anautoa wakati huu akiwa ametangaza hali ya dharula nchini mwake kutokana na hali ya ukame unaoshuhudiwa.

Akizungumza na viongozi wenzake kutoka jumuiya ya SADC katika kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao kuzungumzia athari zilizosababishwa na El Nino, Hichilema alisema kuna haja ya kuwa na umoja kukabiliana na majanga ya kibinadamu yanayosababishwa na tabia nchi.

Kiongozi huyo amezionya nchi wanachama dhidi ya kukabiliana na hali hiyo kibinafsi, akisisitiza kuwa athari za El Nino hazijasaza taifa lolote la ukanda na kwamba kuunganisha nguvu kwa pamoja kutasaidia kudhibiti madhara zaidi.

Aidha viongozi wengine walioshiriki mkutano huo, wameonya kuhusu mdororo wa uchumi unaosababishwa na athari za tabia nchi wakitaka jumuiya ya kimataifa na nchi za ukanda kufanya kazi pamoja kubadili hali iliyopo.

Nchi zilizoathiriwa zaidi na majira ya El Nino ni pamoja na Zambia, Malawi na Zimbabwe, ambazo zimeshatangaza hali ya dharura.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live