Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yawapokea makumi ya wakimbizi kutoka Libya

Rwanda Yawapokea Makumi Ya Wakimbizi Kutoka Libya Rwanda yawapokea makumi ya wakimbizi kutoka Libya

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Rwanda imepokea wakimbizi na waomba hifadhi 91 kutoka Libya chini ya mpango unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya.

Wanajumuisha Wasudan 38, Waeritrea 33, Wasomali 11, Waethiopia saba na Wasudan Kusini wawili.

Wakimbizi hao na wanaotafuta hifadhi walihamishwa chini ya mpango Dharura wa Usafiri wa Dharura, ambao umeshuhudia wakimbizi 2,150 wakipelekwa Rwanda kutoka Libya tangu 2019.

Kati ya hawa, 1,600 wamekwenda kuishi Marekani na kote Ulaya.

"Rwanda itaendelea kujitolea kutoa hifadhi kwa watu wanaohitaji," wizara ya usimamizi wa dharura ya nchi hiyo ilisema Alhamisi.

Kuwasili kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi kunakuja wakati Uingereza ikijaribu kupitisha sheria mpya ambayo itairuhusu kupelekwa kwa baadhi ya waomba hifadhi nchini Rwanda, ikisubiri kushughulikiwa kwa madai yao.

Mahakama ya Juu ya Uingereza hapo awali ilifutilia mbali mpango huo, na kuutaja kuwa ni kinyume cha sheria.

Chanzo: Bbc