Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yasitisha shughuli ya kuwatafuta watu 6 waliotoweka mgodini

Rwanda Yasitisha Shughuli Ya Kuwatafuta Watu 6 Waliotoweka Mgodini Rwanda yasitisha shughuli ya kuwatafuta watu 6 waliotoweka mgodini

Mon, 8 May 2023 Chanzo: Bbc

Serikali ya Rwanda inasema imesitisha kuwatafuta watu sita walioanguka kwenye mgodi huko Kinazi wilayani Huye kusini mwa nchi hiyo siku 16 zilizopita, baada ya msako wa kuwatafuta kutofaulu.

Naibu msemaji wa serikali Alain Mukuralinda alisema kuwa "Serikali ya Rwanda imefanya kila iwezalo kuwatafuta bila mafanikio ".

Waliouawa ni wanaume sita wenye umri wa kati ya miaka 20 na 48, wakiwemo wanafunzi Moïse Irumva, Samuel Nibayisenge na Emmanuel Nsengimana wanaosomea shule ya Goupe Scolaire Kinazi

mgodi huo upo kilomita 3 kutoka shule hiyo.

Mwezi uliopita, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai iliwakamata watu 10 akiwemo Meja [mstaafu] Paul Katabarwa – anayedhaniwa kuwa mmiliki wa mgodi huo haramu, kwa kuhusika kwao na tukio hilo.

Wiki hii, mmoja wa viongozi wa tarafa eneo hilo, ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliiambia BBCkwamba "kazi [ya kuwatafuta] ilienda pole pole kwa sababu mgodi ulikuwa unafikia mahali pa kuangukia waliokuwa katika juhudi za uokozi".

Katika ujumbe wake kwenye Twitter, Mukuralinda alisema kuwa Jumamosi Katibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Assumpta Ingabire, alikutana na familia zilizopoteza watu kwenye mgodi huo.

“Walikubaliana kuachana na juhudi za kuendelea kutafuta watu hao kwa sababu baada ya siku 16 hakuna bahati tena ya wao kuwa hai,” alisema.

Mukuralinda alisema katika kikao hicho pia wamebaini kuwa “kuendelea kuchimba ambapo wamefikia kina cha mita 70 pia ni hatari kwa mazingira”.

Aliongeza kuwa wafiwa wameamua kufanya maombolezi kuanzia Jumamosi hadi Jumapili hii, “na kesho tarehe 9/5/2023 watafanya mazishi”.

"Serikali inalichukulia kwa uzito na imedhamiria kuwa karibu nanyi," alisema.

Mukuralinda ,lakini hakusema lolote kuhusu jinsi watakavyozikwa au iwapo mgodi huo ndio utageuzwa kuwa kaburi lao.

Chanzo: Bbc