Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yaridhishwa na utendaji wa Bandari ya Dar

E9723a61ba4edb740b808b71d7fdd5f2 Rwanda yaridhishwa na utendaji wa Bandari ya Dar

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI ya Rwanda imeridhishwa na utoaji huduma katika Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania na kuahidi kuendelea kuitumia bandari hiyo ambayo imekuwa ikihudumia zaidi ya asilimia 80 ya mizigo ya nchi hiyo.

Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Meja Jenerali Charles Karamba aliyasema hayo mjini Dodoma Desemba 17, 2020 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.

Balozi Karamba amesema kuwa Tanzania na Rwanda si nchi jirani pekee, bali ni ndugu wa damu na Rwanda inaiona bandari ya Dar es Salaam kama bandari ya Rwanda.

Katika mazungumzo hayo pia Balozi Karamba alitumia fursa hiyo kumfahamisha Profesa Kabudi juu ya uwepo wa mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Commonwealth) unaotarajiwa kufanyika mwezi Juni mwaka 2021 nchini Rwanda ambapo itakuwa fursa nzuri zaidi kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Rwanda kufanya biashara kutokana na uwepo wa mkutano huo.

Naye Profesa Kabudi ameeleza kuwa Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa uwekezaji na biashara kwa nchi jirani na nyingine zinaoitegemea Tanzania kupokea na kusafirisha mizigo yake ambapo Tanzania imekuwa ikitumia ndege za Rwanda kusafirisha minofu ya samaki nje ya nchi wakati ikijipanga kununua za kwake ili kuongeza kasi ya biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Chanzo: habarileo.co.tz