Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yaridhishwa na mageuzi Bandari ya Dar

93ad136217781609fc16e8b39f149046 Rwanda yaridhishwa na mageuzi Bandari ya Dar

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI ya Rwanda imeeleza kuridhishwa na mageuzi makubwa ya kiutendaji, yaliyofanywa na Serikali ya Rais John Magufuli katika Bandari ya Dar es Salaam.

Kutokana na mageuzi hayo, taifa hilo la Afrika Mashariki limeahidi kuendelea kuitumia bandari hiyo kuingiza mizigo yake yote kutoka nje na kusafirisha bidhaa zake kutoka nchini humo kwenda nje ya nchi.

Balozi wa Rwanda nchini, Charles Karamba alisema hayo hivi karibuni jijini Dodoma alipokutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Palamagamba Kabudi.

Balozi Karamba alisema Rwanda itaendelea kupitisha mizigo yake yote katika Bandari ya Dar es Salaam,ambayo inafikia asilimia zaidi ya 80 ya mizigo yote inayoingia nchini humo.

Alisema Tanzania na Rwanda si nchi jirani tu, bali ni ndugu wa damu, hivyo wanaiona Bandari ya Dar es Salaam kama bandari ya Rwanda. Kwa upande wake, Profesa Kabudi alisema Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara kwa Rwanda, ili kurahisisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

“Tanzania itajenga mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara kwa Rwanda na mataifa mengine jirani yanayotegemea Tanzania kupokea na kusafirisha mizigo yao,”alisema.

Profesa Kabudi alisema Tanzania inathamini ushirikiano mzuri wa kibiashara uliopo kati yake na Rwanda, ndio maana mpaka sasa inatumia ndege za Rwanda kusafirisha minofu ya samaki nje ya nchi.

Hata hivyo, alisema Tanzania inajipanga kununua ndege yake ya mizigo ili kuimarisha biashara katika nchi za Afrika Mashariki.

Chanzo: habarileo.co.tz