Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yapeleka misaada ya kibinadamu Ukanda wa Gaza

Rwanda Ndege Gaza Rwanda yapeleka misaada ya kibinadamu Ukanda wa Gaza

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rwanda imetuma misaada ya kibinadamu Ukanda wa Gaza, kuonyesha mshikamano na wananchi wa Palestina waliohasiriwa na kujeruhiwa katika mashambulio ya kinyama ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya eneo hilo.

Ndege ya mizigo ya shirika la ndege la Rwanda iliyobeba shehena ya tani 16 za dawa, chakula na maji, ilitua nchini Jordan siku ya Ijumaa ikiwa katika safari ya kupeleka msaada huo Ukanda wa Gaza, Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Msaada huo unatarajiwa kufika Gaza kupitia Misri kutokana na mzingiro uliowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuzuia kufikishwa misaada ya moja kwa moja katika eneo hilo kutokea Jordan.

Siku ya Ijumaa Umoja wa Mataifa ulisema, umesimamia na kufanikisha makubaliano ya kutumwa malori 20 ya awali ya msaada kuingia Ukanda wa Gaza kupitia kivuko cha Rafah kutoka Misri, ikiwa ni mara ya kwanza kupelekwa misaada katika eneo hilo lililokatiwa maji, umeme, chakula na dawa na utawala wa Kizayuni tangu vilipoanza vita Jumamosi ya tarehe 7 Oktoba. Misaada ya kibinadamu inayopelekwa Ukanda wa Gaza

Msemaji wa serikali ya Rwanda Bi Yolande Makolo amesema, serikali hiyo, kupitia Shirika la Msaada la Hashemite la Jordan kwa niaba ya Serikali ya Ufalme wa nchi hiyo, imetoa msaada wa kibinadamu kwa watu wa Palestina huko Gaza.

Bi Makolo ameongeza kuwa, mchango huo wa kuunga mkono juhudi za utoaji misaada zinazoendelea kufanywa kimataifa ulipokelewa mjini Amman siku ya Ijumaa, tarehe 20 Oktoba na unajumuisha tani 16 za vyakula, ikiwa ni pamoja na vyakula vilivyorutubishwa kwa ajili ya watoto, madawa na vifaa vya matibabu.

Mzozo unaoendelea kati ya Wapalestina waliowekewa mzingiro katika Ukanda wa Gaza na utawala haramu wa Israel ambao umegharimu maisha ya maelfu ya watu, umeyagawa mataifa ya Afrika, huku baadhi yao yakiwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina na mengine yakiuunga mkono utawala huo wa Kizayuni.../

Chanzo: www.tanzaniaweb.live