Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yang’ara soko la drone Japan

D7ce5384c80607e5cbb3d7fa20005acf Rwanda yang’ara soko la drone Japan

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SOKO la ndege zisizoendeshwa na rubani za Rwanda limepanuka kutoka bara la Afrika hadi Mashariki ya Mbali katika taifa la Japan.

Baada ya ndege hizo zinazotengenezwa na kampuni ya Zipline kufanya vizuri katika bara la Afrika, kampuni hiyo sasa imeingia mkataba wa ushirikiano na kampuni ya Toyota Tsusho ambayo ni mwanachama wa kampuni kubwa la Toyota ya Japan.

Kutokana na mkataba huo, ndege za ‘drone’ za Rwanda zitatumika nchini Japan kusafirisha dawa katika maeneo yasiyofikika kirahisi kwa kutumia usafiri wa kawaida kama magari.

Ingawa mmiliki wa kampuni hiyo ni Mmarekani, shughuli zake zote za kuzalisha ndege pamoja na bidhaa nyingine zinafanyika Rwanda.

Kampuni hiyo kwa sasa inatoa huduma zake katika vituo vya afya 260 kote nchini, ikiwa na lengo la kufikia zaidi ya vituo vya afya 700 nchini kote.

Ushirikiano huo unatarajiwa kuinufaisha Rwanda kutokana na kukua kwa soko lake la ndege hizo ambazo zinatarajiwa pia kutumiwa na mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Chanzo: www.habarileo.co.tz