Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yalalamikia ukosoaji wa Marekani juu ya vurugu DR Congo

Rwanda Yalalamikia Ukosoaji Wa Marekani Juu Ya Vurugu DR Congo Rwanda yalalamikia ukosoaji wa Marekani juu ya vurugu DR Congo

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Rwanda imeikosoa Marekani kwa kuikosoa kutokana na kuongezeka kwa ghasia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huku ikieleza "wasiwasi wake mkubwa" juu ya kile inachokiita kuachwa kwa mchakato wa amani wa kikanda.

Katika taarifa ya wizara ya mambo ya nje, Rwanda pia inasema jumuiya ya kimataifa haijali "kujengeka kwa kijeshi" DR Congo, na kuongeza kuwa operesheni kubwa ya nchi hiyo katika eneo lake la mashariki mwa Kivu Kaskazini ni kinyume na maamuzi yaliyotolewa na taratibu za kikanda.

Wanajeshi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wamekuwa wakilisaidia jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huku likikabiliana na msururu wa makundi yenye silaha ikiwa ni pamoja na M23.

Wiki iliyopita, wanajeshi wawili wa Afrika Kusini ambao ni sehemu ya vikosi vya SADC waliuawa na watatu walijeruhiwa baada ya bomu la kutengenezea ardhi kutua katika kambi yao.

Mwishoni mwa juma, Marekani ililaani madai ya Rwanda kuunga mkono vikosi vya M23 vya Kongo na kuitaka nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuondoa mara moja majeshi yake yote kutoka DR Congo.Rwanda inakanusha kuunga mkono M23.

Taarifa ya msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliitaka Rwanda "kuondoa mifumo yake ya makombora ya kutoka ardhini hadi angani nchini DR Congo, ambayo ilisema inatishia maisha ya raia, walinda amani na safari za ndege za kibiashara.

Rwanda inasema taarifa ya Marekani inapotosha , na kuongeza kuwa hatua za DR Congo zinatishia usalama wake na ina haki ya kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya tishio hili.

Inasema itatafuta ufafanuzi kutoka kwa Marekani kwani taarifa hiyo inakinzana na mchakato wa kujenga imani ulioanzishwa na Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa wa Marekani mwaka jana.

Chanzo: Bbc