Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yakosolewa kwa kuliunga mkono kundi la M23, DRC

Rwanda Yakosolewa Kwa Kuliunga Mkono Kundi La M23, DRC Rwanda yakosolewa kwa kuliunga mkono kundi la M23, DRC

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: Voa

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa taarifa kwamba waasi wa M23 nchini DRC waliwaua wanavijiji pamoja na watu kutoka makundi yenye silaha mashariki mwa nchi, kati ya mwezi wa Novemba mwaka jana na Aprili mwaka huu, na kisha kuizika miili yao kwenye makaburi ya jumla, wakati Rwanda ikilaumiwa kuwaunga mkono waasi hao.

Human Rights Watch inaeleza kwamba kundi la M23 linaloongozwa na wa Tutsi na kuungwa mkono na Rwanda lilifanya mashambulizi kwenye miji yenye wakazi wengi mashariki mwa Congo mwaka uliopita, na kupelekea majibu kutoka kwa wanajeshi wa kikanda.

Maelfu ya watu wamelazimika kukimbia mapigano hayo karibu na mpaka wa Rwanda na Uganda. Human Rights Watch imesema mashambulizi kwa kutumia milipuko katika maeneo yenye watu wengi katika jimbo la Kivu Kaskazini yameuwa na kuwajeruhi raia, kuharibu miundo mbinu katika nchi ambayo tayari ina hali mbaya ya kibinadamu.

Makundi yenye silaha yanayoipinga M23 pia yamefanya vitendo vya ubakaji. Human Rights Watch imesema Rwanda imepeleka wanajeshi mashariki mwa Congo kutoa misaada ya moja kwa moja ya kijeshi kwa ajili ya M23 , kuwasaidia kueneza udhibiti zaidi Rutchuru na mji jirani wa Masisi.

Shirika hilo limetoa wito kwa serikali ya Congo kupata msaada kutoka Umoja wa mataifa na Jumuiya ya Afrika kuchimbua kwa makini, kurejesha mabaki kwa familia na kuwawajibisha wahusika .

Mwaka jana Umoja wa Mataifa ulililaumu M23 kutokana na vifo vya takriban watu 131 wakati wa ghasia za kulipiza kisasi kati ya kundi hilo na makundi hasimu yenye silaha.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa baadaye ilisema kwamba watu 171 waliuwawa katika siku 10 za mwisho za Novemba mwaka jana.

Aprili na Mei mwaka huu baada ya kundi hilo kuondoka mji wa Kishishe, Human Rights Watch lilitumia picha, video,mashuhuda pamoja na picha za satellite kufichua makaburi 14 ya halaiki.

Kulingana na ripoti ya Jumatano HRW limesema kwamba hayo ni baadhi tu ya makaburi yaliyopo, wakati likiomba ufukuaji wa miili zaidi ufanywe pamoja na uchunguzi kutokana na mauaji hayo.

Hata hivyo M23 imekanusha madai hayo na badala yake kusema kwamba nia ya HRW ni kuwaharibia jina. HRW pia imeunga mkono madai ya Congo, wataalam wa UN pamoja na Marekani kwamba Rwanda inaunga mkono kundi la M23.

Chanzo: Voa