Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yakanusha kuwafukuza Wachina nchini

Kagame Paul Kagame, Rais wa Rwanda

Thu, 16 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Rwanda imelazimika kukanusha taarifa za uzushi ambazo zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii zikidai kwamba Rais Paul Kagame ameamuru raia 18 wa China wafukuzwe kutoka nchini humo.

Ujumbe wa kupotosha uliochapishwa kwenye Twitter ukiwa na madai hayo umesambazwa karibu mara elfu kumi.

Lakini madai hayo si ya kweli, na isitoshe si mara ya kwanza kutolewa kwani yalikuwa yanasambazwa miaka miwili iliyopita.

Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo amesema madai hayo ni ya uzushi akimjibu mwandishi wa Afrika Kusini kwenye Twitter.

Na si mara ya kwanza kwa Bi Makolo kulazimika kuandika ujumbe akipuuzilia mbali madai hayo.

Wakati madai sawa na hayo yaliposambaa mwaka 2020, alilazimika kuandika ujumbe kusema ni ya kupotosha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live