Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yafunga mji mkuu Kigali kufuatia ongezeko la maambukizi ya COVID-19

8cba510497588e8d Rwanda yafunga mji mkuu Kigali kufuatia ongezeko la maambukizi ya COVID-19

Thu, 15 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Idadi ya vifo na maambukizi nchini Rwanda imeongezeka mara dufu huku serikali ikitangaza marufuku ya kutoka nje ya muda wa siku 10 katika mji mkuu wa Kigali na wilaya nane.

Serikali ya nchi hiyo imewataka raia wake kutotoka nje ya nyumba kuanzia siku ya Jumamosi Julai 17 mpaka Julai 26 ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya COVID-19.

Raia watakaotoka nje ni wale wa kupeana huduma muhimu pekee ikiwemo madaktari na walinzi.

Biashara, shughuli za umma na usafiri, shule zote, michezo na maeneo ya burudani pia yamefungwa ila kwa muda usiojulikana.

Hafla za mazishi zitahudhuriwa na watu wasiozidi 15.

Kulingana na wizara ya Afya, Rwanda inashuhudia wimbi la tatu la virusi vya Delta ambavyo nimewaangamiza mamia ya raia.

Kufikia siku ya Jumatano, Julai 14, Rwanda ilikuwa imerekodi visa zaidi ya 50,000 vya virusi vya covid na zaidi ya waathirika 600 na zaidi ya watu 400 wamepata chanjo ya kupunguza makali ya virusi hivyo.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke