Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yafikisha 10% ya chanjo

Rwandani.png Rwanda yafikisha 10% ya chanjo

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali nchini Rwanda imesifiwa kufikisha lengo la kuchanja chanjo ya Corona walau asilimia 10% ya raia wake.

Kufanikiwa kwa hatua hiyo imepelekea nchi ya Rwanda kuondolewa katika orodha ya nchi zilizo chini ya mstari mwekundu wa kuingia katika Nchi za Ulaya.

Mnamo mwezi Agosti hadi Septemba 24, Taifa hilo lilipokea Dozi ya Chanjo Millioni 3.4 , watu 1,466,966 walipata chanjo kamili huku wengine 2,029,038 wakipata dozi moja .

Aidha Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) Afrika kimesema hadi sasa Bara hilo limetoa chanjo kwa asilimia 4.06%. huku Nchi zinazoongoza kutoa Chanjo ya Corona ni Morocco, Afrika Kusini, Algeria pamoja na Tunisia

Chanzo: www.tanzaniaweb.live