Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yaanza kampeni ya chanjo dhidi ya virusi vya Marburg

Ugonjwa Pic Marbug Rwanda yaanza kampeni ya chanjo dhidi ya virusi vya Marburg

Mon, 7 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rwanda imeanza kutoa chanjo dhidi ya virusi vya Marburg tangu Jumapili Oktoba 6, 2024, gonjwa ambao umesababisha vifo vya watu 12 kati ya wagonjwa 41 walioorodheshwa nchini humo tangu mwisho wa mwezi uliopita. Dozi 700 zinazotumwa na taasisi ya utafiti ya Marekani zimekusudiwa watu walio hatarini zaidi na ambao bado wako katika awamu ya majaribio.

Rwanda imezindua mara moja chanjo ya wagonjwa waliotambuliwa na wafanyikazi wa afya, wale walio katika hatari zaidi ya kuambukizwa homa ya Marburg. Siku ya Jumamosi Rwanda ilipokea, kutokana na usaidizi wa kifedha kutoka kwa utawala wa Marekani, dozi 700 kutoka kwa Taasisi ya Marekani ya Sabin Institute, chanjo ambayo bado iko katika majaribio ya awamu ya 2 nchini Uganda na Kenya. Lakini pia tiba za majaribio kutoka kwa maabara ya Californian Mapp.

Hakuna chanjo yoyote kati ya nne au matibabu yanayotathminiwa na Shirika la Afya Duniani ambayo bado yameidhinishwa au kupasishwa kwa majaribio nje ya maeneo ya mlipuko. Hatua za kipnga kwa wasafiri

Wakati huo huo, maabara ya Gileadi ya Marekani imesafirisha dozi 5,000 za remdesivir. Dawa hii hadi sasa imeonyesha ufanisi wa ndani dhidi ya homa hii.

Akizungumza na waandishi habari mjini Kigali, waziri wa Afya Sabin Nsanzimana amesema zoezi la kuchanja waathiriwa limeanza siku ya Jumapili.

Rwanda ambayo inakabiliwa na hali ya dharura, inaweka mikakati ya kuzuia afya kwa wasafiri.

Kisa cha kwanza cha virusi vya Marburg nchini Rwanda kiligunduliwa mwishoni mwa Septemba, ambapo watu 46 wameambukizwa, 12 wamefariki kutokana na homa hiyo.

Dalili za Marburg ni pamoja na homa kali, maumivu makali ya kichwa, uchovu ndani ya siku saba za kuambukizwa, kichefuchefu, kutapika na kuharisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live