Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda ya sita duniani mapambano ya corona

F32cd9729e716ec531f98c30738c284b Rwanda ya sita duniani mapambano ya corona

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

RWANDA imeshika nafasi ya sita duniani kati ya nchi zinazoshughulikia vema mlipuko wa ugonjwa wa covid-19.

Mafanikio hayo yanaelezwa yanatokana na nchi hiyo kuwa na idadi ndogo ya watu na taasisi madhubuti. Ripoti ya taasisi ya The Lowy imetoa orodha ya nchi 98, huku New Zealand ikiongoza na kufuatiwa na Vietnam, Taiwan, Thailand, Cyprus, Rwanda, Iceland, Australia, Latvia, na Sri Lanka.

Katika orodha hiyo, Marekani imeshika nafasi ya 94 ikiwa ni kati ya nchi zinazofanya vibaya huku ikiwa imefanya vema kuliko nchi za Iran, Colombia, Mexico na Brazil.

Utafiti huo haukuhusisha nchi ya China kwa sababu haikutoa viwango vyote vya upimaji ugonjwa huo kwa umma na kueleza masuala muhimu waliyoangalia kuwa ni pamo jana na idadi ya walioambukizwa, vifo na mengineyo.

Rwanda ni kati ya nchi zinazotumia roboti katika vituo vya kushughulikia ugonjwa huo ili kupunguza muingiliano kati ya watoa huduma na wagonjwa wa corona hivyo kupunguza hatari ya kuambukizana.

Chanzo: habarileo.co.tz