Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda namba moja kwa mazingira bora Afrika

Screenshot 2021 08 15 At 11.00.24 660x400.png Rwanda namba moja kwa mazingira bora Afrika

Sun, 15 Aug 2021 Chanzo: millardayo.com

Taifa la Rwanda linaloongozwa na Rais Paul Kagame limeshika namba moja kwa mara ya nne mfululizo katika kumi bora ya Nchi zenye mazingira safi zaidi Afrika.

Namba (10) Namibia (9) Botswana (8) Morocco (7) South Africa (6) Misri (5) Algeria (4) Mauritius (3) Gabon (2) Tunisia na namba moja ni Rwanda ambayo inatajwa kuwa na Watu milioni 12, utafiti huu umefanywa na Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Yale na Columbia wakishirikiana na World Economic Forum.

Wataalamu hao wanasema Nchi ambazo zina hewa safi hazipo kwenye hatari ya kuwa na mazalia ya Wadudu ambao wanaweza kusababisha magonjwa ambayo yana uhusiano na uchafuzi wa hali ya hewa yakiwemo magonjwa ya mfumo wa upumuaji na magonjwa ya moyo.

Chanzo: millardayo.com