Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda na DRC zakubaliana kusitisha mapigano mashariki mwa Congo

Drc Rwanda Angola.jpeg Rwanda na DRC zakubaliana kusitisha mapigano mashariki mwa Congo

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa DRC kuanzia Agosti 4 ya mwezi ujao katika mkutano uliofanyika mjini Luanda Angola.

Hayo yametangazwa na ofisi ya rais wa Angola, nchi ambayo imekuwa mpatanishi katika duru kadhaa za mazungumzo ya kumaliza uhasama kati ya Kongo DR na Rwanda kuhusiana na vita vinavyoendelea mashariki mwa Kongo.

Angola imekuwa mpatanishi katika mzozo mashariki mwa DRC katika jimbo la Kivu Kaskazini, ambapo waasi wa M23 wamekuwa wakipambana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwishoni mwa 2021.

“Mkutano wa mawaziri kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Rwanda, uliofanyika leo (Jumanne) mjini Luanda chini ya upatanishi wa Jamhuri ya Angola, umekubaliana kuanzishwa kwa mchakato wa kusitisha mapigano utakaoanza kutetekelezwa kuanzia saa sita usiku tarehe 4 Agosti,” ofisi ya rais wa Angola ilisema.

Usitishaji mapigano huo utafuatiliwa na kamati maalumu ya kufuatilia utekelezwaji wa makubaliano hayo, iliongeza ofisi hiyo ya Rais wa Angola.

Ghasia zinazoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinazohusishwa na makundi mbalimbali ya waasi, hasa wa M23, zimesababisha mamilioni ya watu kuyahama makazi yao, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu OCHA.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikimtuhumu jirani yake Rwanda kuwa inaliunga mkono kundi la waasi wa M23, madai ambayo yanakanushwa na Kigali, lakini yanaungwa mkono na Marekani, Ufaransa, Ubelgiji pamoja na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live