Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda kutengeneza chanjo ya Uviko-19

Rwanda Covid 19 Rwanda kutengeneza chanjo ya Uviko-19

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Habari la VOA limesema kampuni ya kutengeneza chanjo za Uviko-19 ya BioNtech inalenga kuanza kutengeneza chanjo kwenye kiwanda chake cha chanjo cha mRNA kilichopo nchini Rwanda.

Taarifa iliyotolewa na maofisa wa kampuni hiyo jana, Jumatatu, Desemba 18, 2023 walisema watakuwa kampuni ya kwanza ya kigeni kutengeneza chanjo hizo barani Afrika.

“Vifaa vya kwanza vya kutengeneza kiwanda hicho viliwasili Machi mjini Kigali wakati vikianza kuunganishwa na kuunda mitambo inayojulikana kama BionNtainers,” imeeleza taarifa ya VOA.

BioNTech imesema kwamba kiwanda hicho cha kwanza huenda miaka ya baadaye kikatanuka na kuanza uzalishaji kwenye mataifa mengine ya Afrika yakiwemo Senegal na Afrika Kusini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi uliofanyika jana, Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema chanjo mbalimbali za mRNA ikiwemo ya Uviko-19, kifua kikuu na malaria zinaweza kuzalishwa Kigali na hivyo kukuza wigo wa ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Rais Kagame pia amekipongeza Kituo cha Afrika cha Kudhibiti Magonjwa (CDC), kwa kuratibu ushirikiano wa utengenezaji wa chanjo.

Ikumbukwe Uviko-19 ni ugonjwa ulioibuka mwaka 2019 unaweza kuathiri mapafu, mkondo wa hewa na viungo vingine na husababishwa na virusi vinavyojulikana Korona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live