Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda kupiga kura leo kuchagua Rais

Paul Kagame Mdz Rwanda kupiga kura leo kuchagua Rais

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Julai 15, 2024 Wanyarwanda wameitwa kupiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabunge na Urais uchaguzi ambao Rais wa sasa Paul Kagame anapewa nafasi kubwa ya kushinda tena.

Hakuna kitu kikubwa ambacho kimesubiriwa katika uchaguzi huo wa Urais wa Rwanda ikilinganishwa na ushindi alioupata wa asimilimia 99 mwaka wa 2017.

Frank Habineza kutoka katika Chama cha kisiasa cha kupambania Demokrasia na Mgombea binafsi Philippe Mbayimana wote waligombea kwa mara nyingine tena baada ya kushindwa katika uchaguzi uliopita.

Mwanasiasa kutoka kambi ya upinzani, Diane Rwigara alimnyoshea kidole Rais wa Rwanda Paul Kagame kuwa kizingiti katika kinyanganyiro cha Urais nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live