Wizara ya Afya ya Rwanda imetangaza kampeni ya upandaji miti inayolenga kupanda miti milioni 2 ndani na karibu na vituo vya afya nchini humo.
Waziri wa Afya wa Rwanda Bw. Sabin Nsanzimana amesema kwenye video iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, kuwa mpango huo unaoitwa “hospitali ya kijani” unalenga kubadilisha vituo vya afya kuwa maeneo ya kijani ambayo yanahimiza ulinzi wa mazingira na matokeo bora ya afya.
Amesema miti itapandwa ndani na karibu na hospitali 56, vituo vya afya 514 na vituo vya afya 1,252 kote nchini. Hadi sasa takriban miti 20,000 sasa imepandwa nchi nzima. Amesema kampeni hii iliyozinduliwa katika wilaya ya Bugesera itatekelezwa pamoja na Wizara ya Mazingira ya Rwanda.