Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda kufungua tena viwanja vya ndege Agosti Mosi

RWANDAIRR Rwanda kufungua tena viwanja vya ndege Agosti Mosi

Sun, 5 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rwanda imetangaza Jumamosi kwamba itafungua tena viwanja vyake vya ndege kuanzia mwanzoni mwa Agosti.

"Viwanja vya ndege vya Rwanda vitafungua tena shughuli za ndege za abiria Agosti mosi, 2020'', Wizara ya Miundombinu imesema.

Mwezi Machi, Rwanda ilisitisha huduma zote za ndege zinazoingia na zinazotoka isipokuwa tu kwa ndege za kubeba mizigo na zinazotumika kwa hali ya dharura kwasababu ya janga la virusi vya corona.

Katika taarifa, Wizara ya Miundo Mbinu imesema kwamba abiria wote wakiwemo wale wanaounganisha safari zao kuelekea nchi zingine watahitajika kuonesha kibali kinachothibitisha kwamba hawana virusi vya corona kutoka kwenye maabara iliyoidhinishwa.

Cheti hicho lazima kioneshe kuwa msafiri alifanyiwa majaribio ndani ya saa 72 tangu alipoingia Rwanda.

"Kuhakikisha usalama na afya kwa abiria, wahudumu na wafanyakazi wengine, shughuli kwenye viwanja vya ndege zinazingatia miongozo ya Wizara ya Afya na mapendekezo kutoka kwa Baraza la uimarishaji wa shughuli za ndege," taarifa hiyo imesema.

Aidha, wizara hiyo imeongeza kwamba abiria wanaoingia Rwanda watafanyiwa tena vipimo.

"Kwa abiria wanaoingia Rwanda, watafanyiwa tena vipimo pindi tu watakapowasili, huku matokeo yakitolewa ndani ya saa 24 na katika kipindi hicho watakuwa kwenye hoteli zilizotengwa kwa gharama zao wenyewe," serikali imesema.

Hatua hii ndio ya hivi karibuni kuchukuliwa na Rwanda katika kufungua uchumi wake kwa awamu baada ya tangazo la katikati ya Juni la kufungua shughuli za utalii na kuanza tena kwa safari za kimataifa kwa wanaotumia ndege za kukodi.

Rwanda ilifunga shughuli zake za ndege Machi 2020, na kufunguliwa tena kwa watalii wanaotumia ndege binafsi na kukodi Juni 17, 2020.

Serikali ya Rwanda aimeahidi kuendelea kuufahamisha Umma kuhusu hatua za kuchukuliwa kwasababu hali ya janga la virusi vya corona inabadilika badilika.

Hatua hii imeiweka Rwanda mbele kati ya nchi za Uganda na Kenya ambazo bado hazijafungua shughuli zake za ndege.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live