Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda kuendelea na mapambano dhidi ya wanamgambo nchini Msumbiji

FI1Nwx7XEAES CD Rwanda kuendelea na mapambano dhidi ya wanamgambo nchini Msumbiji

Wed, 12 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanajeshi wa Rwanda wanatarajiwa kuendeleza mapambano dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu nchini Msumbiji, kufuatia makubaliano kati ya nchi hizo mbili kuongeza muda kuhudumu wa kikosi hicho.

Karibu wanajeshi 1,000 wa Rwanda walipelekwa nchini humo mwezi Julai mwaka jana wakati wapiganaji wa kijihadi walipofanya mashambulizi katika maeneo tofauti na kuteka miji katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado.

Hatua hiyo ilipata mafanikio kwa kiwango fulani dhidi ya wanamgambo hao lakini mashambulizi na utekaji nyara wa mara kwa mara unafanyika, waandishi wa habari wanasema.

Mateka 30 waliokolewa wiki hii katika wilaya ya Nangade, mamlaka za Msumbiji zinasema, ufanisi huo ulifikiwa kufuatia oparesheni ya pamoja ya wanajeshi kutoka mataifa mengine ya Kusini mwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live