Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda inavyotumia ndege zisizo na rubani kupambana na malaria

Rwanda Inavyotumia Ndege Zisizo Na Rubani Kupambana Na Malaria Rwanda inavyotumia ndege zisizo na rubani kupambana na malaria

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Rwanda Nchi ya Kwanza barani Afrika Kutumia teknolojia ya ndege zisizo na rubani katika juhudi za kupambana na malaria.

Ndege hizo zinanyunyiza dawa za kuuwa mbu katika maeneo ya mabonde,kwa mujibu wa Taasisi ya Taifa ya Afya (RBC).

Tangu kuanzishwa kwa matumizi ya teknolojia hiyo mwaka 2021, ugonjwa wa malaria ulipungua kwa zaidi ya asilimia 90% katika maeneo yanayofanyiwa majaribio.

Bwana Kamali Paul, ambaye ni msimamizi wa ugonjwa wa malaria katika kampuni ya Charis, anasema wanatumia ndege hizo kwa sababu teknolojia yake inaruhusu kunyunyiza dawa katika eneo kubwa sana na kwa muda mfupi

''kabla ya kunyunyiza dawa kwanza ndege hii inatengeneza ramani ambayo inatusaidia kujua hasa sehemu yenye maji machafu yenye mayai ya mbu.sehemu hii ya kilimo cha mpunga huwa ni kiini cha mbu unaosababisha malaria.tukishapata picha hiyo inaturahisishia kazi ya kunyunyiza dawa.halafu inanyunyiza katika eneo kubwa na kwa muda mchache’’alisema

Kampeini ya kunyunyiza dawa za kukabiliana na mbu imeleta hali ya afueni miongoni mwa wakazi wa maeneo hayo waliozungumza na BBC waliokuwa wamezongwa na malaria.

''Malaria sasa ni historia kwangu.Mimi pamoja na watoto tulikuwa tumezongwa na malaria.Binafsi nilikuwa naugua malaria kama mara tatu ndani ya mwezi moja lakini tangu waanze kunyunyiza dawa,sijaugua ama kuuguza malaria tena imepita miezi mitatu sasa.’’Alisema Bi Musabyima.

Kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Afya (RBC), maeneo ambayo hunyunyiziwa dawa za kukabilia na mbu unaosababisha malaria huchaguliwa kwa sababu ya kuenea kwa ugonjwa huo.

Kwa takwimu, Dk Emmanuel Hakizimana, ambaye anasimamia udhibiti wa malaria katika wizara ya afya anasema kuwa vita dhidi ya Malaria kwa kutumia ndege zisizo na rubani vinaleta matokeo ya kuridhisha katika maeneo ''tunayofanyia majaribio''

‘’Kwa kweli mafanikio ni makubwa –kwanza mbu unaosababisha malaria ulipungua kwa zaidi ya asilimia 85 kadhalika malaria ilipungua kwa zaidi ya asilimia 90.

Hakika matumizi ya ndege zisizo na rubani yamekuja kusaidia sana mkakati tuliokuwa nao wa kunyunyiza dawa kwenye majumba ya watu na pia matumizi ya vyandarua'' alisema Dk Hakizimana

Wizara ya afya ya Rwanda imesema inapanga kupanua kampeini ya kunyunyiza dawa dhidi ya mbu unaosababisha malaria kwa kutumia ndege zisizo na rubani katika wilaya nyingine tano zinazokabiliwa na ugonjwa huo.

Chanzo: Bbc