Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda: WFP inavyolisha watoto mashuleni

Chakula Wfp Mashuleni.jpeg Rwanda: WFP inavyolisha watoto mashuleni

Sun, 30 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkakati wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wa kulisha watoto shuleni umesababisha mabadiliko makubwa katika maisha ya watoto wa shule nchini Rwanda.

Mpango huo ambao umetekelezwa kwa mafanikio katika wilaya saba nchini Rwanda hugawa vyakula bora kwa watoto mashuleni na hivyo kuimarisha elimu, afya na usalama wa miili yao. Lengo la mpango huo wa kugawa chakula kwa wanafunzi mashuleni ni kuhakikisha kila mtoto anapata mlo kamili wenye virutubisho bora kila siku hadi kufikia mwaka 2030.

Wakati huo huo Rwanda imechukua nafasi ya uongozi katika Muungano wa Kimataifa wa Ugawaji Chakula Mashuleni, kundi linalojumuisha nchi 78 duniani na washirika 86 ambao wanaunga mkono mipango endelevu ya chakula mashuleni na kusisitiza ajenda ya mtaji wa rasilimali watu.

Ikiwa ni nchi mwanachama wa muungano huo, serikali ya Rwanda inasema, imejitolea kugharamia chakula cha shule kwa wanafunzi wote. Ahmareen Karim Mkurugenzi wa WFP nchini Rwanda amepongeza juhudi hizo za serikali ya Kigali akisema kuwa, Rwanda inasifiwa sana kwa jinsi ilivyotumia bajeti ya serikali katika miaka michache iliyopita. Hata hivyo mpango wa kitaifa wa kulisha wanafunzi shuleni bado unakabiliwa na vikwazo vya bajeti, na ili kukabiliana na jambo hili, Rwanda imepunguza michango ya wazazi na kupunguza kodi kwenye mchele na mahindi ili kupunguza gharama ya chakula cha wanafunzi mashule na kuhimiza vyanzo vingi vya protini za wanyama kwenye mlo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live