Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda: Mahakama Uingereza kutoa uamuzi wake kuhusu mpango wa wahamiaji

Wahamiaji Rwanda Mahakama.png Rwanda: Mahakama Uingereza kutoa uamuzi wake kuhusu mpango wa wahamiaji

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya juu nchini Uingereza imesema wiki ijayo itatoa uamuzi ikiwa Serikali inaweza kuendelea mbele na mpango wake wenye utata kuhusu kuwapeleka nchini Rwanda, wakimbizi na waomba hifadhi walioko nchini humo.

Uamuzi huo utatolewa baada ya wizara ya mambo ya ndani kuwasilisha rufaa kupinga uamuzi wa awali wa mahakama ya rufaa uliobainisha kuwa mpango wa kuwatuma waomba hifadhi nchini Rwanda ni kinyume cha sheria.

Iwapo uamuzi huo utakwenda kinyume cha matarajio ya serikali, waziri mkuu Rishi Sunak anatarajiwa kuwa chini ya shinikizo toka kwa chama chake ambacho kinataka nchi yao ijiondoe kwenye Mkataba wa Ulaya kuhusu haki za binadamu, ECHR.

Aidha, iwapo mahakama itahalalisha mpango huo, wizara ya mambo ya ndani inatumai ndege ya kwanza ya kuwasafirisha wahamiaji inaweza kuanza safari ya kuelekea Kigali mapema mwakani.

Mpango wa Serikali umekuwa ukipingwa vikali na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu, wanaodai Rwanda haiwezi kuwa nchi salama kwa wakimbizi na wahamiaji hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live