Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda: Kesi mauaji ya halaiki yafungulia Paris

HUKUMU Rwanda: Kesi mauaji ya halaiki yafungulia Paris

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya sita inayohusishwa na mauaji ya halaiki ya Watutsi nchini Rwanda imefunguliwa nchini Ufaransa: daktari wa zamani wa Rwanda, Sosthene Munyemana, anayetuhumiwa kushiriki katika mauaji hayo mwaka 1994, amefikishwa leo Jumanne mbele ya Mahakama ya Paris.

Akiwa chini ya uangalizi wa mahakama, daktari huyu aliyestaafu wa masuala ya uzazi, mwenye umri wa miaka 68, alichelewa kufika kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi iliyopaswa kuanza saa 9:00 asubuhi. Akiwa amevalia shati la mistari ya bluu na koti la kijivu, aliomba msamaha kwa kuchelewa, kabla ya kufichua utambulisho wake.

Anakabiliwa na kesi ya mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binadamu, kushiriki katika makubaliano kwa nia ya kuandaa uhalifu huu, pamoja na kujihusisha, na anakabiliwa na kifungo cha maisha. Anapinga shutma dhidi yake. Kesi hiyo, iliyopangwa kwa wiki tano, itarekodiwa kama sehemu ya uhifadhi wa kumbukumbu za kihistoria za mahakama. Uchunguzi wa muda mrefu

Hii ni kesi kongwe zaidi kuchunguzwa nchini Ufaransa, kwa jina la mamlaka ya kimataifa ya haki ya Ufaransa, juu ya ukweli unaohusishwa na mauaji haya ya kimbari ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 800,000 kati ya mwezi Aprili na Jmwezi ulai 1994, kulingana na Umoja wa Mataifa: malalamiko ya kwanza dhidi ya Sosthène Munyemana, ambaye aliishi kusini-magharibi mwa Ufaransa baada ya mauaji mwaka huo, aliwasilishwa Bordeaux (kusini-magharibi) mwaka 1995, na kusababisha kufunguliwa kwa uchunguzi wa mahakama.

Urefu wa uchunguzi unaelezewa hasa na "haja ya kufanya uchunguzi nje ya nchi", "uundaji wa kitengo cha uhalifu dhidi ya binadamu" cha mahakama ya Paris mnamo mwaka 2012 tu, na "kuzuia uhusiano wa kitaasisi kati ya Ufaransa na Rwanda kati ya mwaka 2009 na 2012", alieleza kwa kina Mkuu wa Mahakama, Marc Sommerer.

Daktari huyo wa magonjwa ya wanawake, ambaye anachukuliwa kuwa mtu mashuhuri katika eneo la Butare (kusini mwa Rwanda), anashukiwa kuchangia katika kuandaa pendekezo la kuunga mkono serikali ya mpito iliyoanzishwa baada ya shambulio la ndege ya rais Juvénal Habyarimana, ambaye alichochea mauaji hayo. Anawasilishwa kama mtu wa karibu na Jean Kambanda, Waziri Mkuu wa serikali ya mpito.

Pia anatuhumiwa kushiriki katika kamati ya mgogoro ambayo iliweka vizuizi na eneo ambapo watu walikamatwa kabla ya kuuawa. Hatimaye, anatuhumiwa kushikilia ufunguo wa ofisi ya sekta ya Tumba, ambapo Watutsi walifungwa, wakati mwingine kwa siku kadhaa na katika "mazingira yasiyo na heshima", kulingana na mashtaka, kabla ya kunyongwa. "Ukweli wa mahakama"

Sosthène Munyemana alisema wakati wote wa uchunguzi kuwa ofisi ya sekta hiyo ilitumika kama "kimbilio" la Watutsi ambao walikuwa wakitafuta mahali pa ulinzi. "Tungependa (...) itambulike kuwa Daktari Munyemana sio tu kwamba hakushiriki kwa njia yoyote ile katika mauaji ya halaiki, lakini yeye mwenyewe alitishiwa pakubwa na wauaji wa mauaji hayo kwa vile alikuwa Mhutu mwenye msimamo wa wastani", amewaambia waandishi wa habari Wakili Jean-Yves Dupeux, ambaye anamtetea mtuhumiwa huyo akishirikiana na Wakili Florence Bourg.

Kwa jumla, zaidi ya watu 110 na mashirika 8 wamejiunga kama vyama vya kiraia kwa ajili ya kesi hiyo, na karibu mashahidi 70 watasikilizwa.

Alipowasili Ufaransa ambako mkewe alikuwa tayari anaishi Septemba 1994, baba wa watoto watatu, Sosthene Munyemana, daktari wa magonjwa ya wanawake, alifanya kazi kama daktari wa dharura kusini-magharibi kabla ya kujielekeza upya katika matibabu ya watoto. Akiwa analengwa na hati ya kimataifa ya kukamatwa iliyotolewa na mamlaka ya Rwanda, ombi lake la kupata hifadhi lilikataliwa mwaka 2008, lakini vyombo vya sheria vya Ufaransa vilikataa mwaka 2010 kumrejesha nyumbani ili aweze kuhukumiwa nchini mwake.

Wanaume sita - watumishi watatu waandamizi wa serikali, afisa, askari na dereva - tayari wamehukumiwa nchini Ufaransa kwa kushiriki kwao katika mauaji ya halaiki, hadi vifungo vya kuanzia miaka 14 ya kifungo cha uhalifu hadi kifungo cha maisha. Watatu kati yao bado hawajahukumiwa katika mahakama ya Rufaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live