Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda: Jean Baptiste Mugimba ahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa mauaji ya halaiki

Rwandaaaaaaaa Jean Baptiste Mugimba na wakili wake

Fri, 18 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama katika Mji wa Nyanza nchini Rwanda imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 25 jela dhidi ya Jean Baptiste Mugimba, Katibu wa zamani wa Muungano wa Kutetea Haki za Jamhuri (CDR) ,muungano unaoshutumiwa kuwa na itikadi kali za kisiasa mwaka 1994 nchini Rwanda .

Mahakama imemkuta na hatia ya kupanga na kutekeleza mauaji katika mitaa ya mjini Kigali.

Baada ya hukumu hiyo kutangazwa amekata rufaa .Bwana Mugimba alirejeshwa Rwanda kutoka Uholanzi mwezi Novemba 2016.

Mahakama ilimpata na hatia Mugimba ya kutenda jinai kwa kuongoza kikao cha dharura nyumbani kwake tarehe 8 April mwaka 94 ,kikaokilichopanga mauaji dhidi ya watutsi katika mtaaNyakabanda mjini Kigali .

Jean Baptiste Mugimba, mfanyakazi wa zamani wa Benki Kuu ya Rwanda ambaye alikamatwa na Uholanzi na kupelekwa Rwanda mwaka 2016, katika kesi yake alikana mashtaka dhidi yake.

Kadhalika mahakama ilimpata na hatia ya kugawa silaha kwa wanamgambo na kuamuru kuweka vizuizi barabarani ili kuwazuia watutsi waliokimbia kutoroka mauaji hayo.

Ni ushahidi ambao wakati wa vikao vya kesi hii Bwana Mugimba na wakili wake walipinga.

Mugimba alisema mashahidi walijichanganya katika kutoa hojazao na kwamba yeye siku inayotajwa ya kikao hicho alikuwa amehamia mtaa mwingine na kudaimashtaka dhidi yake yalipangwa maksudi na watu ambao walitaka kumnyanganyamali yake.

Alisema hakuwa na mamlaka yoyote ya kuitisha kikao kinachodaiwa kushirikishabaadhi ya maafisa wa jeshi na viongozi wengine.

Mugimba mwenye umri wa miaka 65 alikuwa katibu mkuu wa muungano wa kutetea Jamuhuri ‘The Coalition for the Defence of the Republic’ kinachoshutumiwa kuwa na itikadi kali dhidi ya watutsi. Mahakama ilisema alikuwa namamlaka na ushawishi wa kutosha kuongoza wananchi na wanamgambo kufanya mauaji.

Kwa mjibu wa sheria Kosa la kupanga na kutekeleza mauaji ya kimbari linatolewa hukumu ya kifungo cha maisha,lakini jaji amesema mahakama imeamua kumpunguzia hukumu hiyo na kumpa kifungo cha miaka 25 jela kutokana na mwenendo wake mahakamani.moja kwa moja ametangaza kukata rufaa akipinga hukumu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live