Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda:'Hatuna matumaini ' watu 10 waliozama Nyabarongo bado wako hai

Rwanda:'Hatuna Matumaini ' Watu 10 Waliozama Nyabarongo Bado Wako Hai Rwanda:'Hatuna matumaini ' watu 10 waliozama Nyabarongo bado wako hai

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Mamlaka nchini Rwanda inasema bado inawatafuta watu 10 wengi wao wakiwa watoto waliokuwa kwenye mashua iliyozama katika mto Nyabarongo.

Boti iliyokuwa na watu 14 (13 na mpiga kasiawake) ilizama majira ya saa 15:00 jioni (17:00) siku ya Jumatatu, watatu kati yao na mpiga kasiawa boti hiyo, ndio walionusurika, wakati wa shughuli ya uokoaji iliyofanywa na wananchi.

Gavana wa jimbo la kusini, Alice Kayitesi, aliiambia Radio ya taifakuwa leoshughuli za uokoajizinaendeleakukiwa nausaidizi wa polisi wa majini lakini kuwapata wengine wakiwa hai "hakuna matumaini kabisa’’

BBC ilijaribu kuwasiliana na gavana wa jimbo la kusini ambaye alisema alikuwa katika eneo la milimani kwenye matatizo ya mawasiliano ya simu.

Magazeti nchini Rwanda yanasema kuwa ajali hiyo ilitokea katika sehemu ya mto huu, Mushishiro, wilayani Muhanga, na kwamba waliokuwa kwenye boti hiyo walikuwa na umri wa kati ya miaka 9 na 13.

Gavana Kayitesi alisema kuwa boti hiyo haikukidhi mahitaji ikiwa ni pamoja na kuwa na injini, waliokuwemo kutovaa jaketila kuokoa maisha na ukosefu wa bima.

Ofisa huyo alisema maji ya Nyabarongo yaliishinda boti hiyo na kusababisha kupinduka katika mto huo katika sehemu iliyo karibu na Bwawa lilojengwa kwenye mto wa Nyabarongo.

Ajali za boti katika Mto Nyabarongo zimekuwa za mara kwa mara kwa miaka 10 iliyopita, huku mamlaka mara nyingi ikisema kuwa zinasababishwa na botizilizozeeka nazilizojaa kupita kiasi.

Baadhi ya wakazi wa Mto Nyabarongo hutumia safari za boti kama njia nafuu na ya haraka kufika katika baadhi ya maeneowanakofanyia kazi na ambako siyo rahisikufika wakitumia njia ya nchi kavu.

Chanzo: Bbc