Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda: Hatujakata tamaa na kusitishwa safari ya ndege ya waomba hifadhi

Rwanda Wakimbizi Ndege Hatujakata tamaa na kusitishwa safari ya ndege ya waomba hifadhi

Thu, 16 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rwanda "haijakata tamaa" baada ya safari ya kwanza ya ndege iliyopaswa kuchukua waomba hifadhi kutoka Uingereza kuwapeleka nchini humo kuahirishwa, kwa mujibu wa msemaji wa serikali.

Hadi watu saba walikuwa wanatarajiwa kusafirishwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Lakini safari ya ndege ilisitishwa baada ya uingiliaji kati uliochelewa kutoka kwa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR) kusababisha changamoto mpya katika mahakama za Uingereza.

"Hatukatishwi tamaa na yaliojiri. Rwanda inasalia kujitolea kikamilifu kufanya ushirikiano huu ufanye kazi. Hali ya sasa ya watu wanaofanya safari za hatari haiwezi kuendelea kwani inasababisha mateso yasiyoelezeka kwa wengi," msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo alisema.

"Rwanda iko tayari kuwapokea wahamiaji hao watakapofika na kuwapa usalama na fursa katika nchi yetu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live