Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda Air yasitisha safari zake za Mumbai

Rwanda Air Rwanda Air yasitisha safari zake za Mumbai

Sun, 3 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Ndege la Rwanda (RwandAir), litasitisha safari zote za Ndege kwenda na kurudi Mumbai, kuanzia Machi 15,2024 ikiwa ni katika mkakati wake wa kuboresha huduma.

Akizungumzia ni kwa nini Shirika la Ndege hilo linapanga kusimamisha safari ya kuelekea jiji lenye watu wengi zaidi nchini India, Kaimu Afisa Mkuu wa Biashara wa RwandAir (CCO) Andrew Best Owie aliliambia gazeti la The New Times kwamba: “RwandAir ilianza safari zake miaka saba iliyopita, na imeendelea kuangalia njia mpya kuboresha utoaji wa huduma katika njia nzuri.

RwandAir imekuwa ikifanya safari zake katika miji zaidi ya 20 Magharibi, Kati, Mashariki na Kusini mwa Afrika, Mashariki ya Kati, Asia na Ulaya, kulingana na taarifa kutoka kwa Shirika hilo la ndege.

Barani Afrika Rwand Air imekuwa kifanya shughuli zake katika maeneo ya Abuja, Accra, Bangui, Brazzaville, Bujumbura, Cape Town, Cotonou, Dar es Salaam, Douala, Entebbe, Harare, Johannesburg, Kilimanjaro, Lagos, Libreville, Lusaka, Nairobi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live