Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto sababu za kupungua mwili

Ruto Sababu Za Kupungua Mwili Ruto sababu za kupungua mwili

Mon, 15 May 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Kenya William Ruto anasema kupunguza uzani wake unaoonekana ni juhudi zake za makusudi za kujiweka sawa huku kukiwa na wasiwasi wa baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii kuhusu afya yake.

Akizungumza katika mahojiano na wanahabari Jumapili, Rais Ruto alieleza kuwa ameongeza uzito katika kipindi cha kampeni mwaka wa 2022.

Wakati huo, alisema, kulikuwa na shinikizo kubwa ambalo wakati mwingine lilisababisha mkazo wa kula.

Bw Ruto alisema alipunguza uzito baada ya kuanza tena programu yake ya utimamu wa mwili, lishe na afya njema.

“Kwa asili ya kazi yangu, sina budi kuwa macho,” akasema Bw Ruto.

Baadhi ya Wakenya walikuwa wameona kuwa Rais Ruto alikuwa amepungua uzito miezi kadhaa baada ya kuchukua wadhifa wa mtangulizi wake.

Wengine walikisia kwamba huenda mkuu huyo wa nchi alikuwa mgonjwa.

Chanzo: Bbc