Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto na Uhuru waingiwa na wasiwasi kuhusu uamuzi wa mahakama Ijumaa

30b8dfcfcc010925 Ruto na Uhuru waingiwa na wasiwasi kuhusu uamuzi wa mahakama Ijumaa

Tue, 17 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mahakama ya Rufaa Ijumaa Agosti 20 itatoa uamuzi wake kuhusu rufaa ya BBI baada ya majaji saba kuskiza pande zote mbiliNi uamuzi ambao unasubiriwa kwa hamu na pande za kisiasa za handisheki na Tangatanga kwani utakuwa na athari za kisiasaUpande ambao hautaridhika utakuwa na nafasi ya kuenda katika mahakama ya upeo kutafuta haki zaidiIjumaa Agosti 20 ni siku ambayo inasubiriwa kwa hamu na kambi za kisiasa za Tangatanga na Handisheki huku mahakama ikisubiriwa kutoa uamuzi kuhusu BBI.

Mahakama ya Rufaa inatarajiwa kutoa uamuzi wake baada ya upande wa Handisheki kukata rufaa kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Juu ulioitupa nje BBI.

Rufaa hiyo iliskizwa kuanzia Juni 29 hadi Julai 2 na kikosi cha majaji saba ambao wamekuwa wakiandika uamuzi wao.

Rais wa mahakama ya rufaa Daniel Musinga alisema kikosi hicho kitatoa uamuzi wake Agosti 20 ili kujua iwapo reggae itanedelea.



Mahakama ya Juu ilitupa nje BBI ikisema ilikosa kufuata sheria na hivyo haiwezi kusonga mbele na kufanyiwa refarenda.



Katika uamuzi wa majaji wa Mahakama ya Juu, mswada wa BBI ulianzishwa na Rais Uhuru Kenyatta ambapo ni kinyume cha sheria.

Wakereketwa wa BBI hata hivyo hawakukubaliana na hilo huku wakiambia Mahakama ya Rufaa kuwa Junet Mohammed na Dennis Waweru ndio walikuwa waanzilishi wa mswada huo.



Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga wamekuwa katika mstari wa mbele kushabikia mswada huo wakisema utakuwa na manufaa makubwa kwa nchi.

Rais wakati wa ziara yake Kisumu mwezi Mei alisema anaamini kuwa wanasheria sugu kama vile Seneta James Orengo watasaidia kuokoa jahazi la BBI.

“Nikon a imani tukiwa na mawakili kama vile James Orengo tutashinda hii kesi iko mahakamani,” Uhuru alisema wakati wa ziara yake.

Kwa upande mwingine, Naibu Rais William Ruto na kikosi chake wamekuwa wakisherekea kutupwa nje kwa BBI wakisema lengo lake ni kuwatafutia viongozi fulani mamlaka.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke