Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto kupunguza bajeti safari za nje

Kenya: Ruto Afanya Mabadiliko Katika Baraza La Mawaziri Rais Ruto

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya Dkt. William Ruto amesema Serikali yake imepunguza bajeti ya usafiri wa nje ya nchi kwa KSh11 bilioni (≈ Tsh bilioni 186) baada ya ukosoaji wa umma juu ya ziara zake nyingi nje ya nchi. Dkt Ruto amesema watumishi wa umma hawataruhusiwa kuhudhuria warsha nje ya nchi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo cha uongezaji thamani ya vito vya Voi na uuzaji katika Kaunti ya Taita Taveta, Dkt Ruto ameagiza kwamba bajeti za usafiri kwa mihimili yote mitatu ya Serikali zipunguzwe kwa 50%.

“Tumepunguza bajeti ya usafiri kwa KSh11 bilioni katika wizara au idara zote na sio KSh50 milioni zilizoripotiwa na vyombo vya habari. Hakutakuwa na makongamano ya nje, warsha, ‘bench marking’ kwa watumishi wa umma,” alisema Ruto.

“Nimepunguza ile pesa ya kurandaranda na kuzunguka....niliona watu wa gazeti jana wakisema nimepunguza na milioni mia tano....hapana, nimepunguza na bilioni kumi na moja,” alisema Rais Ruto.

“Pesa ya Wakenya haiwezi kwenda kununua marinda...Ati wanaenda bench marking, ati wanaenda kununua viatu...sasa tumesema kwamba safari yoyote itakuwa ile ya kuletea Wakenya faida tu,” amesema Rais Ruto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live