Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto kuhutubia Wakenya huku kukiwa na shinikizo kutokana na mafuriko makubwa

Ruto Kuhutubia Wakenya Huku Kukiwa Na Shinikizo Kutokana Na Mafuriko Makubwa Ruto kuhutubia Wakenya huku kukiwa na shinikizo kutokana na mafuriko makubwa

Fri, 3 May 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Kenya William Ruto anatarajiwa kuhutubia taifa huku kukiwa na shinikizo kubwa la kutangaza mafuriko makubwa yanayoendelea kuwa janga la kitaifa.

Msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed, ambaye alitoa tangazo hilo, hakutoa maelezo kuhusu hotuba hiyo leo Ijumaa.

Lakini Rais Ruto anatarajiwa kuzungumzia mvua kubwa inayoendelea kunyesha ambayo imeua takriban watu 188 tangu Machi na kusababisha mamia kwa maelfu kuyahama makazi yao.

Hotuba hiyo inajiri siku moja baada ya baraza la mawaziri kuonya kuwa eneo la pwani huenda likakumbwa na kimbunga, kikiambatana na mvua kubwa, mawimbi makubwa na upepo mkali unaoweza kuathiri shughuli katika Bahari ya Hindi.

Baraza la Mawaziri, ambalo lilikutana kwa mara ya pili wiki hii, pia lilisema kuwa mvua za wastani hadi juu ya wastani zitaendelea kunyesha kote nchini.

Serikali imeamuru watu wanaoishi karibu na mabwawa kuhama mara moja au kulazimishwa kuhamia maeneo salama.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ametoa wito kwa rais kutangaza mafuriko hayo kuwa janga la kitaifa ili kuandaa njia ya kuungwa mkono na kimataifa.

Nchi jirani ya Tanzania, ambako takriban watu 155 wameuawa katika mafuriko na maporomoko ya ardhi, pia inatarajiwa kuhisi nguvu ya Kimbunga Hidaya.

Chanzo: Bbc