Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto awataka Uhuru na Raila kuomba msamaha

269932898f6d3ca2 Ruto awataka Uhuru na Raila kuomba msamaha

Fri, 3 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ruto alisema Raila na Uhuru wamekuwa wakirindima siasa za BBI kwa miaka mitatu licha ya kuwaambia yaliyomo hayafaiAlisema wanafaa kuomba msamaha baada ya mahaka kutupa nje msaa huo kwa kuwa kinyume cha sheriaKuanguka kwa BBI kulionekana kuwa ushindi mkubwa kisiasa kwa DP Ruto na wandani wake katika siasa ya kuelekea Ikulu 2022Naibu Rais William Ruto Alhamisi Septemba 2 aliwataka Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga kuomba msamaha kwa Wakenya kuhusu BBI.

Ruto alisema kwa miaka mitatu Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM wamekuwa wakirindima siasa za BBI jambo alilosema lililemaza huduma kwa raia.

Alisema serikali ilikuwa kwenye harakati za kuchapa kazi ili kubadilisha maisha ya wananchi lakini ikatekwa na suala la BBI.

"Kwa bahati mbaya tukapata ajali, tukaletewa reggae na BBI. Sasa ile mipango ya kubadilisha maisha ikasimama kwanza. Ikasemekana tuendeni kwanza tukabadilishe katiba," alisema.

Aliendeleza kampeni zake dhidi ya mswada huo wa mabadiliko ya kikatiba akisema ulikuwa wa kuwanufaisha viongozi.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke